📌NA DOTTO KWILASA
KUELEKEA
uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuanza Oktoba 28 mwaka huu,wanawake wametakiwa
kujitoa kuwachagua viongozi Wenye maono ya kuwaunganisha wanawake na
dunia.
Wito
huo umetolewa na wanawake
wajasirimali Katika Jukwaa la "Mwanamke Shujaa Tanzania"
linaloendelea Katika uwanja wa kumbukumbu ya mwalimu Nyerere"Nyerere
Square"jijini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Jukwaa hilo mkoa wa Dodoma Peris Privatus amesema ikiwa wanawake
watakubali kushiriki kikamilifu Katika uchaguzi mkuu wataweza kuchagua na
kuwapa nafasi viongozi wenye ndoto za kuwaingiza wanawake katika uchumi wa
viwanda na kuwasaidia kujikwamua kiuchumi bila kutegemea kuwezeshwa na wanaume.
Pamoja
na hayo Mwenyekiti huyo wa Mwanamke
Shujaa ameongeza kuwa ili kufika kilele cha mafanikio kwa pamoja,wanawake
wanapaswa kusaidiana kuzifikia ndoto za kila mwanamke mmoja mmoja.
Wanawake wajasiriamali tuna nafasi kubwa katika jamii yetu ya Tanzania na Dunia nzima kwa ujumla,tuna wajibu wa kuwahamasisha wanawake wenzetu kujituma na kukubali mafanikio;Kwa kuanza ,tumeleta bidhaa zetu hapa kuonyesha wanawake wenzetu kuwa ni Wakati wa mafanikio ya wanawake na dunia,hakuna kubaki nyuma.
Peris Privatus
Kwa upande wake Katibu wa Jukwaa hilo la Mwanamke Shujaa
Dodoma,Emeryciana Mbulagwisha alisema ingawa baadhi ya wanawake wengi
hawajapata ujasiri wa kuishi kufuatana na matakwa yao, wapo wengine
wanaoishi na kutimiza ndoto zao katika maisha yao kila siku.
Katika mafanikio ya kila mwanamke tunahimiza nguvu ya mwanamke katika jamii tukiamini wanawake wote wanaweza kuchukua nafasi hii kutambua ujasiri na upambanaji wao katika jamiiEmeryciana Mbulagwisha
Licha ya hayo aliongeza kuwa Jukwaa la Mwanamke Shujaa Katika karne hii, lingependa kuona kila mwanamke anapewa kipaumbele na kuwezeshwa katika jamii, jambo litakalosababisha wanawake wengi kujitambua na kufanya mambo makubwa zaidi na kutambulika kimataifa.
Mwanamke mpambanaji ni mwanamke imara na anayeijua nguvu iliyo ndani yake ya kupambana na kukabiliana na changamoto katika nyanja mbalimbali za maisha ili kutimiza malengo yakeEmeryciana Mbulagwisha
Tumaini
Kyando ni mmoja wa wajasirimali Mwanamke Katika Jukwaa hilo ambapo amesema kuwa
licha ya wanawake kukabiliana na changamoto nyingi wanapaswa kuongeza juhudi
bila kuchoka kupambana.
Kyando
aliongeza kuwa ,ili kuwa na wanawake wengi mashujaa lazima kuongeza zaidi
ujasiri katika nafasi za kujiendeleza na kuinuana bila kuoneana wivu wa
maendeleo .
Naye
Several Joseph ametumia nafasi hiyo kuwaaminisha wanawake kwa kusema kuwa mwanamke
jasiri haogopi kushindwa na changamoto zilizo mbele yake, siku zote
huchagua kuzikabili.
Amesema,Wanawake
wengi wajasiri wamefanikiwa kuinua uchumi wao na kuzisimamia familia zao,
wakati mwingine bila hata ya msaada wa mwanaume.
Kila Mwanamke mpambanaji ana ndoto za kuwa mtu fulani ama kufikia malengo fulani,hivyo basi hatupaswi kuogopa kuwa tofauti na mategemeo ya wengineSeveral Joseph
0 Comments