📌NA FAUSTINE GIMU GALAFONE
CHAMA cha wanasheria wanawake
Tanzania (TAWLA),kwa kushirikiana na Taasisi ya vijana TYC,pamoja na WE
EFFECT,wamezindua mradi wa miaka mitatu (3) wa kuongezea
Uwezo kwa ushiriki wa wanawake na vijana katika masuala ya uongozi
Akizungumza katika uzinduzi huo,
uliofanyika leo Jijini Dodoma Mgeni rasmi ambaye ni Msajili wa Mashirika yasiyo
ya Kiserikali Nchini {NGO} kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Bi
Vickness Mayao ametoa wito kwa Wanawake na vijana ambao
watachaguliwa katika nafasi za uongozi kutumia nafasi watakazopata kwa maslahi
ya Taifa.
Aidha amewataka kuzingatia
kanuni na maadili ya uchaguzi kulingana na Sheria za uchaguzi huku akiwataka
TAWLA kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii kuhusu vijana na wanawake kuongeza
ushiriki wa nafasi mbalimbali za uongozi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAWLA,Tike Mwambile akielezea lengo la
mradi huo amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuweza kuongeza usawa wa kijinsia
katika ushiriki wa uchaguzi kwa wanawake na vijana.
Nao washiriki wa mradi huo toka
katika Mikoa ya Arusha na Tanga wametoa maoni yao.
mradi huo ambao unaanza kutekelezwa
mwaka huu wa 2020 hadi 2023 unafanyika katika mikoa mitatu ya
Arusha,Tanga na Mwanza.
0 Comments