WAANDISHI WAASWA 'KUTOWAPA MBELEKO' WENYE AJENDA BINAFSI



📌NA HAMIDA RAMADHANI 

VYOMBO vya Habari nchini vimetakiwa kukataa kutumika na wanasiasa wenye ajenda zao binafsi ambazo hazina msingi kwa Taifa hasakatika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na badala yake vizigatia kanuni, sheria, miongozo na maadili ya uandishi wa habari.

Kauli hiyo imetolewa Leo jijni Dodoma na Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile kwenye mkutano mkuu wa Jukwaa hilo.

Balile amesema katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu vyombo vya habari na wahariri wasikubali kutumiwa na wanasiasa kwa namna yoyote ile ili kulinda taaluma yao.

Amesema inajulikanawazi mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu vyombo  vyote vya Habari vitatenda haki .

Tuwahakikishie watanzania kuwa vyumba vya habari na jukwaa la wahariri hawatatumika kusambaza chuki, matusi na ajenda za watu ambazo hazina msingi wowote kwa Taifa na tutaendelea kutekeleza majukumu yetu ya kitaaluma kwa kuzingatia miongozo na maadili ya kazi yetu na kuviacha vyama vya siasa kufanya siasa na kamwe hatutawasaidia wanasiasa kushinda kwa sababu haitatusaidia kitu chochote
 Balile..

Amesema malalamiko kutoka kwenye vyama vya siasa na wanasiasa mwaka huu yatakuwa mengi lakini vyombo vya habari vinatakiwa kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa kuvipa usawa vyama vyote kusikika.

Kwa upande wake mhariri wa magazeti ya uhuru kanda ya Dodoma, Kiondo Mshana alisema wahariri wasikubali kuandika matusi kutoka kwa wanasiasa kwa kigezo cha kuwapa nafasi ya kusikika na badala yake waandike yale yenye manufaa kwa wananchi.

Amesema hakuna chombo chochote cha habari ambacho kitakuwa tayari kutoa habari zenye lugha chafu, matusi na zisizofaa kwa wananchi kwa kigezo cha kutoa habari zenye usawa kwa wagombea wote mwaka huu.

Ila kama mtu ataeleza ni nini atawafanyia wananchi kwenye sekta ya maji, elimu, afya na miundombinu huyo atapata nafasi kwa sababu atakuwa ametanguliza ajenda ya wananchi mbele na si matusi na kejeli.
Kiondo Mshana.

Naye Mhariri wa gazeti la Mtanzania Kurwa Karedia aesema wanasiasa wanaolalamika kuwa hawatendewi haki na vyombo vya habari wachunguze kauli zao wanazozitoa wanapokuwa jukwaani kwani Mhariri hatapitisha habari ambayo ina mapungufu kwenye chombo chake ya habari.

Amesema habari zote zitakazotoka kwenye vyombo vya habari ni lazima ziwe zimekidhi viwango vya habari kwa kuwa na pande zote (balanced) na siyo habari yenye upande mmoja tu kwa kisingizio Cha uchaguzi mkuu.


Post a Comment

0 Comments