VYOMBO VYA HABARI VYAASWA KUTOINGILIA UHURU NA MAJUKUMU YA TUME YA UCHAGUZI




📌NA HAMIDA RAMADHANI

WAKATI Tume ya uchaguzi ikikamilisha zoezi la Uteuzi wa wagombea wa kiti Cha Rais, Makamu wa Rais ,ubunge na Udiwani nchi nzima Tume imeviasa vyombo vya Habari kuzingatia sheria na maadili ya kazi zao.

Hayo yamesemwa leo jijini hapa  na Mkurugenzi wa Tume wa uchaguzi Dkt.Charles Mahera alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari vinavyotangaza matokeo yauteuzi wa wagombea wa ubunge na Udiwani.
 Vyombo vya habari zingatieni sheria na maadili ya kazi zenu naongea haya kwasababu wakati  Tume ikiwa haijatoa  taarifa yoyote juu ya zoezi hili muhimu, tayari kumeibuka vyombo vya habari kadhaa vimeanza kutangaza matokeo ya Uteuzi huu.
Dkt Mahera.

Na kuongeza kusema 
kuna baadhi ya chombo cha habari asubuhi ya leo kimetoa matangazo ya wabunge inadai kuwa wameshinda kwa kuwa wamepita bila kupingwa majimboni mwao

Amesema kitendo hiko ni kinyume Cha sheria za uchaguzi na kuna maana ya kukopa au kunyan'ganya Uhuru wa na majukumu ya Tume ya Taifa ya Chaguzi.

Aidha amesema kwa mujibu wa kifungu Cha 40 (2) Cha sheria ya Taifa ya uchaguzi,Sura ya 343 , pingamizi linaweza kuwekwa kwa mgombea wa ubunge kama zuio kwa mgombea aliyeteuliwa kuanzia saa 10 :00 jioni siku ya Uteuzi hadi saa 10:00 jioni siku inayofuatia baada ya siku ya Uteuzi.
 Sasa kabla ya muda huo wa kuweka pingamizi haujaisha tayari vyombo vya habari vimeanza kutangaza matokeo haya kinyume Cha sheria , kitendo hiko kinaweza kuchochea vurugu na uhasama miingoni mwa wananchi. 
Hata hivyo ametoa wito kwa jamii na waandishi kwa ujumla kuwavmakini na Habari zinazorushwa mitandaoni.


Post a Comment

0 Comments