📌NA DEVOTHA SONGORWA
MWENYEKITI wa Umoja wa
Wanawake Tanzania, mkoa wa Dodoma, Neema Majule amesema kuwa maandalizi
kuelekea uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28
mwaka huu yamefikia hatua nzuri.
Mwenyekiti huyo amesema
kwamba uamuzi wa kufanyika uzinduzi August 29 katika makao makuu ya nchi ni
heshima kubwa na itatoa picha halisi namna Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kilivyojipanga kushiriki katika uchaguzi kikamilifu.
Uzinduzi huo utafanyika
tarehe 29 mwezi huu kutwa katika Uwanja wa Jamhuri mgeni rasmi akiwa ni Rais,
Dk.John Magufuli.
Amewataka wanawake
kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura kama haki yao kikatiba akisema ni
wakati wao sasa kufanya maamuzi ya kuchagua kiongozi atakayekuwa tayari kutetea
haki za wanawake na kumfanya mwanamke kutambua ana sehemu ya kufanya kufikia
kilele cha mafanikio.
Maandalizi yanaendelea vizuri usafi wa uwanja umefanyika, kutakuwa na wawakilishi kutoka mikoani na unajua huu ni uzinduzi wa kampeni kitaifa, wasanii watakuwepo tumejipanga vizuri sana na vikundi vya hamasa na wanachama wenyewe watakuwepo mambo yamepamba moto
Neema Majule.
Pia Neema ameeleza
kwamba wakati wote wa kampeni wagombea wamejiandaa kufanya kampeni kwa
kuzingatia sheria kwa kunadi sera zao na ahadi zao wa wapiga kura huku akisema
kwamba katika hili vijana hawajaachwa nyuma kwani wana mchango mkubwa katika
Taifa lolote lile hivyo ni wakati wao sasa kuunga mkono chama kwa kuhakikisha
CCM inapata ushindi wa kishindo.
Katika hatua nyingine
aliwataka wagombea hasa wanawake waliojitokeza kuchukua fomu lakini
hawakufanikiwa kuingia katika kinyang'anyiro kutokata tamaa kwani wameonyesha
uthubutu wa hali ya juu hivyo watumie mwanya huyo kuwapa kura waliochaguliwa
kumuwezesha mgombea wa kiti cha Urais Ndugu John Pombe Magufuli kushika tena
miaka mitano kuhudumia watanzania.
Tumefanya kikao cha ndani tukawaita wagombea wote iwe alipita au hakupita karibu wagombea 400 wanawake sasa wameamua na ni jeshi kubwa tumewaomba waende wakahamasishe wanawake wengine kukipigia kura ya ndiyo Chama Cha CCM nafasi zote Rais, Wabunge na Madiwani wanawake tunaweza
Neema Majule.
Akizungumzia makundi
maalumu Mwenyekiti huyo alibainisha kwamba CCM ni Chama ambacho kinakumbatia
makundi maalumu yote bila ubaguzi na kimekuwa kikitoa nafadi za uongozi hata
kwa watu wenye ulemavu akisema wana haki kisheria kama watu wengine kwani
ulemavu wao hauzuii haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa ni kazi kwao kuamini
kwamba wana uwezo mkubwa kufanya mageuzi ya kimaendeleo.
Yaani katika kundi ambalo Chama hiki kinawaangalia kwa jicho la tatu ni watu wenye ulemavu tumeshuhudia Rais wa Awamu ya Tano, Dk.John Magufuli alianzisha asilimia 10 kutoka kila Halmashauri kutoa asilimia 2% kwa wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi kwanini tusimpigie tena kura ya ndiyo mtetezi wa wanyonge.
Neema Majule
Aidha kuhusu vitendo
vya rushwa katika zoezi la uchaguzi amesema kwamba hakuna haki katika rushwa na
CCM ni Chama amacho kinafuata misingi ya sheria na kipo mstari wa mbele kupiga
vita rushwa huku akiwataka wapiga kura nao kutowafumbia macho wagombea
wasiowaminifu.
0 Comments