📌NA.FAUSTINE GIMU GALAFONI
Jeshi la polisi Mkoani Dodoma
limesema limejipanga kwa mashambulizi kwa wale wote watakaokuwa na nia ovu ya
kufanya vurugu na kuhatarisha amani katika kampeni za vyama mbalimbali za
siasa.
Akizungumza na waandishi wa jijini Dodoma Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles
Muroto amebainisha kuwa makundi yote ya ovyo ambayo yamejiandaa kwa ajili
ya kuleta vurugu yatashughulikiwa na kazi ya jeshi la polisi ni kulinda
amani ya Tanzania.
Tanzania huwa naifananisha na mto wa maji mtulivu,mara nyingi huwezi ukaona kwa macho umetulia ndani ya mto huo kuna viumbe maisha yao yanategemea hapo, hivyo hakuna mnyama anayekubali kuchezewa hayo maji kenge wataenda sehemu zao na mamba sehemu zao ikimaanisha kuwa jeshi la polisi halitakaa kimya amani ya Tanzania ichezewe
Aidha,Kamanda Muroto amesema kuwa
jeshi la Polisi litahakikisha linafuatilia kwa makini mwenendo wa kampeni na
kubainisha kuwa Tanzania haina Mjomba wala shangazi nje ya nchi huku
akiwataka waandishi wa Habari kutumia kalamu zao vizuri kuhakikisha hakuna
Habari za uchochezi.
“Tanzania haina mjomba wala
shangazi nje nchi nyingi ambazo zinatuzunguka zimekuwa zikija hapa kwa sababu
zimekuwa zikipata matatizo kwa hiyo sisi kama jeshi la polisi tunahakikisha
tunalinda amani na waandishi wa Habari muwe sehemu ya Watanzania kuhakikisha
hali ya amani na utulivu inakuwepo”amesema.
0 Comments