📌NA FAUSTINE GIMU GALAFONI
Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa hapa nchini,Mhe. John Shibuda ameitaka tume ya taifa ya uchaguzi (NEC)kuhakikisha uchaguzi mkuu Oktoba 28,2020 unafanyika kwa haki na uwazi na usiwe wa madoa kama ilivyotokea uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka jana.
Shibuda amesema hayo Leo Agosti 24,2020 jijini Dodoma katika Kongamano kuu la kihistoria la kuomba dua na sala kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani 2020 lililoandaliwa na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania.
Uchaguzi wa Serikali za mitaa ulikuwa na madoadoa na manung'uniko hall ambayo ilisababisha baadhi ya watanzania kutokuwa na imani ya Serikali yao hivyo nataka madoadoa kama hayo yasijirudie Uchaguzi mkuu uwe wa Haki na wazi.
Shibuda
0 Comments