📌NA HAMIDA RAMADHANI
Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) imetupilia mbali mapingamizi mawili yaliyowekwa na mgombea urais
kupitia Chama cha Demojrasia na Maendeleo(Chadema)Tundu Lissu dhidi ya wagombea
wa nafasi hiyo Dkt.John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi na Profesa Ibrahim
Lipumba wa Chamancha Wananchi (CUF).
Awali akizungumza na
waaandishi wa habari katoka ofisi za Chadema jijini Dodoma kuhusu mapingamizi
hayo Lissu amesema,ameweka mapingamizi mawili dhidi ya Rais Magufuli na
pingamizi moja dhidi ya profesa Lipumba kwa madai kwamba hawajakidhi masharti
na sheria za uchaguzi.
Lissu alitaja
pingamizi la kwanza ambalo linamuhusu Dkt.Magufuli na Profesa Lipumba kuwa ni
kupeleka fomu zao za wadhamini kukaguliwa na kuhakikiwa na wakurugenzi wa
uchaguzi na kisha kugongwa mihuri wakati wenye mamlaka ya kufanya hivyo ni NEC
pekee yake kwa mujibubwa sheria za Tume hiyo.
Pingamizi la pili
linamuhusu Dkt Magufuli peke yake ambalo amedai picha zilizoambatanishwa kwenye
fomu zake siyo zilizohitajika kwa mujibu wa sheria za Tume ya Uchaguzi ambazo
ni picha mdogo (paspot size) lakini mgombea huyo amesema picha zilizopigwa
upande na kwamba kinachoonekana ni nusu sura.
Pingamizi la kwanza ni mgombea kupitisha fomu zake za kutafuta wadhamini kuhakikiwa na kugongwa mihuri na wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo aliowateua yeye na pingamizi hili pia linamuhusu Profesa Lipumba huku akisema ni kinyume cha sheria ya uchaguzi.
Tundu Lissu
Lissu amesema NEC ndiyo yenye
Mamlaka ya kuhakiki wadhamini wote kutoka mikoa 10 Tanzania bara na mikoa
miwili Tanzania Visiwani.
Kufuata mapingamizi hayo ameiomba
NEC baada ya kuwapa muda wa kujitetea waliowekewa mapingamizi iwakutanishe muweka
na wawekewa mapingamizi kwa mujibu wa sheria.
TUME YA UCHAGUZI YATOA MAJIBU
Akitoa uamuzi wa NEC, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Wilson Mahera amesema kuwa NEC kwa kuzingatia masharti ya kanuni 39(5) ya kanuni za uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020, baada kupokea mapingamizi dhidi ya wagombea hao ,iliwataarifu mapema iwezekanavyo na wahusika wamewasilisha utetezi wao kwa Time hiyo.
Akizungumza
mapingamizi dhidi ya Dkt.Magufuli kwamba hakuambatisha picha kwenye fomu za
uteuzi na hakurudisha fomu ya utetezi kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na
sheria, Dkt.Mahera amesema "Tume baada ya kupitia sababu za mapingamizi
imejiridhisha kuwa Dkt.Magufuli amerejesha fomu zake ambazo zimeambatishwa
pamoja na picha kwa mujibu wa sheria ,kanuni na maelekezo ya Tume ,
Hivyo imehiridhisha kwamba mapingamizi hayo hayana msingi wa kisheria na kuyatupilia mbali na kwa maana hiyo Dkt.Magufuli ni mgombea halali wa kati cha Rais kupitia Chama Cha Mapinduzi.Dkt. Mahera
Kuhusu mgombea wa CUF
Dkt.Mahera amesema kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na sheria,Tume baada ya
kupitia sababu ya pingamizi pamoja na utetezi uliotolewa ,imejiiridhisha kuwa
mgombea huyo kupitia Chama cha wananchi (CUF),amerejesha fomu zake kwa mujibu
wa sheria ,kanuni na maelekezo ya NEC.
Hivyo NEC imejiridhisha kwamba pingamizi hilo halina msingi wa kisheria na imelitupilia mbali na kwa hiyo Profesa Ibrahim Lipumba wanaendelea kuwa mgombea halali wa kati cha Rais kupitia Chama cha wananchi (CUF).Dkt.Mahera
Aidha alisema kwa
mujibu wa kanuni ya 39(6) ya kanuni za uchaguzi wa Rais na Wabunge za
mwaka 2020 ,sababu za uamuzi huo wa Tume watapewa kwa maandishi wale wote
walioweka pingamizi wa waliowekewa pingamizi.
0 Comments