📌NA FAUSTINE GIMU GALAFONE
Halmashauri Kuu ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Agosti 20, 2020 imetangaza majina ya wateule
watakaopeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika
Oktoba 28, 2020
Akitangaza
majina ya wagombea makao makuu ya CCM jijini Dodoma,katibu Mwenezi
wa chama hicho Humphrey Polepole amesema waliopitishwa kugombea Ubunge katika
Mkoa wa Shinyanga kwenye uchaguzi Mkuu 2020 ni pamoja na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini , Patrobas Katambi
ambapo atagombea jimbo la Shinyanga Mjini.
Wengine ni
Boniface Butondo jimbo la Kishapu, Idd Kassim jimbo la
Msalala,Elias Kwandikwa jimbo la Ushetu,Jumanne Kishimba jimbo la Kahama
Mjini na Ahmed Salum Jimbo la Solwa.
Katika
mkoa wa Dar es Salaam waliopitishwa kugombea Ubunge kupitia chama hiko ni
pamoja na Aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile katika jimbo
la Kigamboni, Dkt. Josephat Gwajima jimbo la Kawe, Abdallah Chaurembo jimbo la
Mbagala, Dorothy Kilave jimbo la Temeke.
Dkt.
Kitila Mkumbo jimbo la Ubungo, Issa Jumanne Mtemvu jimbo la Kibamba, Jerry Slaa
jimbo la Ukonga, Bona Kalua jimbo la Segerea, Abbad Tarimba jimbo la Kinondoni
pamoja na Mussa Zungu jimbo la Ilala.
Chama
cha Mapinduzi[CCM],kimetangaza wagombea watakaokiwakilisha Chama hicho Kutetea
kiti cha Ubunge katika Majimbo yote 264 hapa nchini Tanzania.
0 Comments