📌NA.FAUSTINE GIMU GALAFONI
MGOMBEA Urais kupitia
chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu ametoa mapingamizi kwa
wagombea wawili kiti cha Urais
Akizungumza na Waandishi wa habari Leo Agosti
26,2020 jijini Dodoma Lissu ametaja waliowekewa pingamizi ni pamoja na mgombea
Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na
mgombea Urais kupitia Chama Cha Wananchi(CUF) Prof.Ibrahim Haruna Lipumba.
Miongoni mwa Mapingamizi aliyotoa Lissu ni
pamoja na pingamizi la kurejesha fomu za wadhamini kabla ya tarehe ya
uteuzi,pamoja ,kusainiwa fomu kwa wakurugenzi badala ya kusainiwa na tume ya
Taifa ya Uchaguzi pamoja na kuweka kuweka passport size isiyokidhi vigezo.
Hivyo,Lissu amesema kwa mujibu wa sheria
wawekewa pingamizi wanapaswa kukutana ana kwa ana na muweka pingamizi katika
ofisi za tume ya Taifa ya uchaguzi jijini Dodoma kujitetea dhidi ya mapingamizi
hayo.
Kuhusu suala la kukatwa kwa majina ya
wagombea udiwani na ubunge wa CHADEMA Lissu amewataka kukata rufaa Mara
moja katika ofisi za tume za majimbo na ngazi za juu za ofisi
za tume ya taifa ya Uchaguzi ili wapate fursa ya kujitetea.
0 Comments