📌NA.FAUSTINE
GIMU GALAFONI
RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli anatarajia kuwa Mgeni Rasmi katika
kongamano la kitaifa la Jumuiya ya Maridhiano litakalofanyika siku ya Jumatatu
Agosti,24,2020 jijini Dodoma.
Akizungumza na Waandishi
wa Habari leo Agosti,21,2020 jijini Dodoma,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano
Tanzania ambayo inahusisha dini zote za wailam na Wakristo,Sheikh Alhad Musa
Salum amesema kongamano hilo litatoa fursa kwa viongozi wote wa dini
kuwasihi wagombea kufanya kampeni za busara zisizo na matusi,Pamoja
na kuhamasisha tume ya Taifa ya Uchaguzi kusimamia haki ili kuendelea kutunza
amani ya Tanzania.
Sisi watanzania ni watu wastaarabu saana hivyo hivyo katika kongamano hilo kutakuwa na miogozo mbalimbali hasa kuwahamasisha wanasiasa kufanya kampeni za busara zisizo na matusi pia tutatoa miongozo kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kusimamia Haki katika uchaguzi mkuu Oktoba 28
Pia
Sheikh Alhad Musa Salum amesema ,katika Kongamano hilo la Amani la
Jumuiya ya Maridhiano mambo mengine yatakayojadiliwa ni elimu kwa wananchi
umuhimu wa ushiriki katika kupiga kura ambapo Zaidi ya wageni elfu kumi
wanatarajia kuhudhuria katika kongamano hilo.
Hivyo,Sheikh Salum
amesema sababu za kufanya kongamano hilo ni baada ya kuona viashiria vingi vya
uvunjifu wa amani vikiwemo kuchomwa moto baadhi ya ofisi za vyama ,matusi na
vijembe baadhi ya wagombea ambapo pia amebainisha kuwa kundi la watu
wenye ulemavu litapewa kipaumbele Zaidi katika ushiriki wa kongamano hilo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Maridhiano Taifa, Sheikh Alhad Musa Salum
Kwa upande wake Katibu
mkuu wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania,Askofu Dkt.Osward Herman Mlay
amesema kuna umuhimu kwa viongozi wa dini kuungana bila kujali itikadi za dini
zao ambapo pia ametoa onyo kwa viongozi wa dini wanaojihusisha na
masuala ya kisiasa katika nyumba za ibaada kwani wanaweza kuhatarisha amani ya
nchi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Maridhiano idara ya wanawake mkoa wa Dodoma Pili Mohammed Yomba amesema kamati
katika mkoa wa Dodoma imejipanga kuwahudumia wageni wanaotoka katika mikoa
mbalimbali ya Tanzania.
0 Comments