📌NA HAMIDA RAMADHANI
WAZIRI wa Mambo ya Nje ya Nchi Profesa Palamagamba Kabudi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kitabu cha historia ya Rais John Magufuli.
Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma
Mwandishi wa kitabu hicho Mathias
Joseph Kabadi amesema kitabu hicho kinaeleza maisha binafsi ya Rais Magufuli kuanzia utoto ,
Siasa, alivyaanza kufanya kazi mpaka sasa alipo.
Uzinduzi wa
kitabu hicho utafanyika tarehe 5 August
mwaka huu katika viwanja vya Nyerere Square jijini hapa.
Kilichonisukuma kuandika historia hii ni kutokana na uwajibikaji wake ,pili kulikuwepo na changamoto juu ya uraia wake zikidai kuwa yeye si mtanzania hivyo kitabu hiki kitasaidia Wananchi kumjua vizuri Rais MagufuliMathias Joseph Kabadi
Amesema kitabu hicho kitauzwa kwa bei ya shilingi 5000
ili kuwezesha kila Mtanzania kusoma kitabu hicho na baada ya uzinduzi kitabu hicho
kitasambazwa nchi nzima ili Watanzania wakisome na kumfahamu Rais Magufuli..
0 Comments