📌NA HAMIDA RAMADHANI
JAMII imeaswa kuendelea kudumisha amani na mshikamo na kuachana na mihemko ya kisiasa katika kipindi hiki cha kuelekea mchakato wa uchaguzi mihemuko ambayo itasababisha machafuko hapa nchini na wananchi wachague viongozi wenye Sera zenye tija kwa jamii.
Akizungumza katika ibada ya Jumapili Askofu kiongozi wa kanisa la International Evangelism Church lilipo Swaswa mkoani Dodoma Mchungaji Thadey Silvester amesema wao kama kanisa liliingia katika mfungo wa siku 21 kwaajili ya kuliombea taifa katika mchakato wa uchaguzi.
Sisi kama kanisa tumeingia katika maombi ya siku 21 kwaajili ya kuweza kuliombea taifa tumeona katika kipindi cha uchaguzi kumekuwa na vurugu vitisho sisi tumeingia katika mfungo huu wa siku 21 kuendelea kupambana na hizi roho chafu
Askofu Thadey
"Nichukue tu fursa hii kusema kwamba watumishi wa Mungu wawapo madhabahuni watumie muda huu kuhubiri amani na si kufanya siasa katika mahubiri lakini pia hatumzuii mtu kuwa mwana siasa isipokuwa achague moja asichanganye vitu viwili kwa pamoja kama tunavyoona kama Mchungaji Gwajima kajitokeza,kugombea lakini pia tulikua na marehemu mama Lwakatare, na kuna Mchungaji Msigwa"amesema Mchungaji Thadey
Aidha kwa upande wake Askofu Dr Israel Gabliel Maasa kutoka Arusha amewataka wananchi hasa katika kipindi hiki cha mchakato wa uchaguzi wawachague viongozi ambao watayaenzi mambo yaliyoachwa na viongozi wengine
Niwaambie tu ndugu zangu tuangalie na tuchague wale viongozi ambao wanajali watu, wanyonge na watakaotetea maslahi ya wananchi
Askofu Dr Israel Gabliel Maasa
WITO KAWA VIONGOZI WA DINI
Aidha Askofu Dkt Maasa ametoa wito kwa viongozi wote wakiroho pindi wanapokuwa madhabahuni wasichanyanye siasa na dini.
" Hili nitatizo kubwa sana kiongozi wa dini hatakiwi kuchukua mambo ya siasa na kuyaleta katika madhabahu hili halifai,"amesema Askofu huyo.
Hata hivyo ameihamasisha jamii na waamini wote wa dini zote waangalie na wachague viongozi ambao wanaleta sera nzuri na si lugha za matusi.
0 Comments