📌NA RHODA SIMBA
JESHI la kujenga Taifa {JKT}
limetangaza nafasi za kujiunga na Jeshi hilo kwa kujitolea kwa vijana wote wa Tanzania
Bara na visiwani huku likisisitiza kuwa
halihusiki na kuwatafutia ajira vijana pale wanapomaliza mafunzo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa tawi la Utawala Kanali Julius Kadawi kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga T
vijana kuomba kujiunga na kuchaguliwa na mafunzo hayo utaratibiwa na
ofisi za Wakuu wa Wilaya na wakuu wa Mikoa
ambapo mwombaji anaishi.
Aidha Kanali Kadawi amesema
maandalizi ya vijana kuomba na mpaka kujiunga na jeshi hilo kwa
kujitolea unaanza mwezi agosti 2020 na vijana watakaoteuliwa wanatakiwa
waripoti kwenye makambi ya JKT mwezi
Oktoba 2020.
“Jeshi la kujenga Taifa linapenda kuwataarifu vijana kuwa
watakaopata fursa hiyo kuwa halitoi
ajira kwa vijana na pia halihusiki na kuwatafutia vijana ajira katika asasi,
vyombo vya ulizni na usalama na mashirika mbalimbali serikali na yasiyo ya serikari bali hutoa
mafunzo ambayo yatawasaidia vijana kujiajiri wenyewew mara tu wanapomaliza
mkataba wao pale tu wanapomaliza mafunzo yao ya Jeshi la kujenga Taifa”
Sifa za mwombaji awe raia wa Tanzania elimu na umri ,vijana wenye elimu ya darasa la saba umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18, na kwa vijana wenye elimu ya kidato cha nne umri usiwe zaidi ya miaka 20 na kwa vijana wa kidato cha sita umri usiwe chini ya miaka 18 na usiwe zaidi ya miaka 22 vijana wenye elimu ya stashahada umri usiwe zaidi ya miaka 25 na elimu ya shahada usiwe zaidi ya miaka 26, na shahada ya uzamili usiwe zaidi ya 30, na shahada ya uzamivu umri usiwe zaidi ya miaka 35
Kanali Kadawi.
Amesema kutokana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu [COVID
19] nchini tahadhali za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kama zilivyoelekezwa
na serikali kupitia wizara ya afya zitazingatia kwa kipindi chote vijana
watakapokua makambini.
Hata hivyo Kanali Kadawi ametoa wito kwa vijana wote watakaopata fursa
hiyo ya kujiunga waitumie ili
wajifunze uzalendo ukakamavu stadi za kazi na stadi za Maisha na pia kuwa tayari kulinda na kulitumikia Taifa.
0 Comments