A
📌HAMIDA RAMADHANI
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji Nchini (EWURA) imetoa
sababau ya kuadimika kwa mafuta kuwa ni kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya
Petroli .
Aidha kuanzia Juni 2020 matumizi ya petroli yaliongezeka kufikia lita
mil.3.683 kwa siku na Julai 2020 matumizi yaliongezeka zaidi kufikia lita
mil.4.425 kwa siku ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 21.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma, Meneja wa
Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo amesema pia bei mpya za mafuta zitaanza kutumika kesho
Agast 5 katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha pamoja na ongezeko hilo amesema akiba ya mafuta iliyokuwepo katika
magahala iliendelea kutosheleza mahitaji ya nchi
Kuanzia Julai 29 hadi 31 Agosti 2020 kuna jumla ya meli sita za petrol zinazotegemewa kupokelewa ambapo kati ya hizo meli tatu zimeshawasili nchini zikiwa na jumla ya lita mil. 89.564 kwaajili ya soko la ndani na zitatosheleza matumizi ya zaidi ya siku 18
Titus Kaguo.
Pia amesema kuwa meli nyingine tatu zitawasili kati ya Agosti 17 na 31
mwaka huu zikiwa na takribani lita mil.100.075 zitakazo tosheleza mahitaji ya
nchi kwa zaidi ya siku 22.
Kwa upande wa mafuta ya Diesel Kagua alisema kuwa yapo yakutosha
na meli tatu za mafuta hayo zenye jumla ya lita mil.193.391 zinategemewa
kuwasili nchini Agosti 2020 ambapo mafuta hayo yatatosheleza mahitaji ya dizeli
kwa zaidi ya siku 30.
“Ili kuwa na utoshelevu wa mafuta nchini,kuanzia Septemba 2020 Ewura
imeongeza makadirio ya matumizi ya mafuta kwa siku kuwa lita mil.4.812 kwa
petrol na lita mil.6.082 kwa dizeli.
“Wakala wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja (PBPA)atatumia makadirio haya
wakati wa kuagiza mafuta,”amesema.
Amesema Petroli itaongezeka kwa shilingi 139 kwa lita kwenye toleo
lilotoka Julai ambapo itakuwa imeongeza kwa asilimia 8.22 huku kwa upande
wa Diesel ikiongezeka kwa shilingi 69 sawa na asilimia 4
Tunakuja na bei mpya kuanzia Jumatano kesho Petroli imeongezeka kwa shilingi 139 kwa lita kwenye toleo lilotoka Julai kwahiyo imeongeza kwa asilimia 8.22 huku Diesel ikiongezeka kwa shilingi 69 sawa na asilimia 4
Amesema kwa Dar es salaam bei ya zamani kwa Petroli ilikuwa
sh.1693 sasa itauzwa kwa sh.1832.
Amesema Mkoa wa Tanga bei imeongezeka kwa shilingi 214 sawa na asilimia
12.94 huku Diesel ikiongezeka kwa shilingi 85 sawa asilimia 5.02.
Amesema Diseli awali ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi 1693 ambapo sasa
itauzwa kwa shilingi 1778 na Petroli awali ilikuwa shilingi 1654 sasa itauzwa
kwa shilingi 1868.
Amesema kwa Mkoa wa Mtwara Petroli imeongezeka kwa shilingi 263 sawa na
asilimia 12.29 huku Diesel ikiongezeka shilingi 68 sawa na asilimia 3.95.
Amesema kwa Mkoa wa Mtwara Petroli itauzwa kwa shilingi 1875 ambapo
awali ilikuwa ni shilingi 1612 huku Diesel ikiuzwa kwa shilingi 1799 ambapo
awali ilikuwa ni shilingi 1731.
Meneja Biashara wa Ewura,Kemilembe Kafanabo |
Akizungumzia sababu za bei kuwa tofauti katika Mikoa ya Tanga na
Mtwara,Meneja Biashara wa Ewura,Kemilembe Kafanabo amesema ni kutokana na bei
kutofautiana katika soko la dunia.
“Kwa Mkoa wa Tanga mafuta mara ya mwisho yalipokelewa katika
Bandari ya Tanga mwezi wa nne mafuta yale yalikuwa na bei ya soko la
dunia ya mwezi wa tatu na sote tunafahamu kwamba bei za soko la dunia
zilianza kushuka kwa kiwango kikubwa kuanzia mwezi wa nne.
“Kwa hiyo bei za kutokea bandari ya Tanga zimedumua kuanzia kipindi kile
hadi leo ndio sababu tunaona kuna ongezeko kubwa katika badari hiyo.
“Kwa Mtwara yalipokelewa kwa vipindi tofauti kuanzia mwezi wa tatu
hivyo kutokana na utofauti mzigo unakuwa na bei tofauti kutokana na kipindi
ambacho kimepokelewa,”amesema Kafanabo
Akizungumzia upande wa usambazaji wa mafuta nchini Kaguo amesema kuwa
kwa kiasi kikubwa changamoto ya upatikanaji wa mafuta ya petrol iliyojitokeza
mwishoni mwa Julai 2020 imechangiwa na kuchelewa kwa meli moja iliyokuwa ifike
nchini kati ya julai 22 na 24 mwaka 2020 na badala yake ikawasili julai 29
mwaka huu.
Kuchelewa kwa meli hii kulitokana na changamoto zilizokuwepo katika
‘refinery’ yalikotokea mafuta hayo na upepo wa Monsoon huko baharini uliyofanya
meli kusafiri kwa kasi ndogo
Amesema kutokana na kuchelewa kwa meli hiyo kwa takribani siku 7,kuna
uhaba kidogo uliojitokeza katika maeneo machache,ambapo Ewura ilifanya
mawasiliano na kampuni za mafuta kuhakikisha mafuta yanapatikana maeneo yote.
Aidha amesema kuwa usambazaji wa mafuta kwa sasa nchini niwakuridhisha
na maeneo yote yana mafuta ya kutosha isipokuwa maeneo machache.
“Hali ya upatikanaji wa mafuta Kanda zilizo chini ya Ewura ni
pamoja na Kanda ya Mashariki inayojumuisha mikoa ya Dar es
salaam,Mtwara,Lindi,Pwani na Morogoro ambapo mafuta yanapatikana bila
matatizo,”amesema.
Vilevile Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya
Tanga,Arusha,Kilimanjaro na Manyara mafuta yanapatikana bila matatizo,na Kanda
ya kati inayojumuisha mikoa ya Dodoma,Tabora,Singida na Iringa pia yanapatikana
bila matatizo.
Kanda ya Nyanda za juu kusini inayojumuisha mikoa ya Ruvuma,Njombe,Mbeya,Songwe,Rukwa na Katavi ambapo mafuta yanapatikana isipokuwa kuna uhaba ulijitokeza katika Mji wa Mpanda mkoani Katavi na hata hivyo kuna lita 37,000 ambazo zimeanza kuuzwa na kuna lita 100,000 ziko njiani zikitegemewa kuwasili leo jioni.
Hata hivyo amesema kuwa Kanda ya Ziwa inayohusisha mikoa ya
Mwanza,Mara,Simiyu,Kagera na Kigoma mafuta yanapatikana isipokuwa kuna uhaba
umejitokeza katika Wilaya za Bunda na Musoma mkoani Mara.
“Hii inatokana na kuchelewa kuondoka kwa magari ya mafuta kutoka Dar es
salaam kuelekea maeneo hayo hasa kwa kuzingatia kuwa kulikuwa na siku tatu
ambazo siyo za kazitangui ijumaa ya julai 31 mwaka huu.
“Mafuta yamekwishapakiwa na yako njiani kuelekea katika maeneo husika
ikitegemewa mafuta hayo yatafika kati ya leo na kesho,”amesema.
0 Comments