DIWANI MTEULE KILIMANI ARUDHISHA FOMU



📌NA BARNABAS KISENGI

DIWANI Mteule kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Kata ya Kilimani Neema Mwaluko amerudisha fomu ya uchaguzi katika ofisi za tume zilizopo katika ofisi ya Kata ya Kilimani jijini Dodoma ambapo amekamilisha masharti na vigezo vyote vilivyotakiwa na tume ya uchaguzi.

Bi Mwaluko amesema anakishukuru chama chake kwa kumwamini tena kupeperusha bendera katika kipindi kingine cha 2020-2025 ili akawatumikie wananchi wa Kata ya Kilimani.

Kwa upande wake msimamizi msaidizi wa Kata ya Kilimani FatumaAamri amesema katika Kata ya kilimani waliojitokeza kuchukuwa fomu za tume kuwania nafasi ya udiwani wa Kata hiyo ni wanachama wa vyama viwili tu. 


Pamoja na Neema Mwaluko aliyerudisha fomu ya tume majira ya saa 5:36 asubuhi na John mgombea mwingine ni Jerome Chami kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)  ambaye naye amerudisha fomu ya tume majira ya saa 6:05 na wote wamekamilisha vigezo vyote vilivyotakiwa na tume ya uchaguzi ili kushiriki uchaguzi mkuu ujao.

Post a Comment

0 Comments