📌NA BARNABAS KISENGI
MKUU
wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Jabir Shekimweri amemuagiza Mkuu wa Polisi
wilaya hiyo (OCD) kuwakamata viongozi wa kijiji cha Kibodiani wilayani hapo kwa
kushindwa kumkamata kijana wa kijiji hicho kwa tuhuma za kulima bangi.
Kijana
huyo ambaye jina lake halikuweza kutambulika mara moja anatuhumiwa kulima bangi
zaidi ya ekari moja katika eneo la
milima ya kijiji hicho.
Akiongozana
na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya katika ziara ya kutembelea
maeneo hayo.Shekimweri aliamuru shamba hilo litekeketezwe baada ya kubainika
uwepo wa mihadarati hiyo.
Shekimweri baada ya
kuliteketeza shamba hilo, amemuagiza Mkuu huyo wa Polisi kuhakisha anamkamata mwenyekiti wa kijiji
hicho na viongozi wengine kwa uzembe na kutobaini uwepo wa shamba hilo.
DC Shekimweri amesema viongozi
hao watawajibika kwa kumlinda kijana huyo na kutanabaisha kwamba shamba hilo
lipo karibu na barabara wanayopita viongozi hao wa kijiji kila siku na wakiwa
wanaiona lakini wamefumba macho.
Serikali ipo na ina mkono mrefu kwa wale watakao kuwa wanajishughulisha na kilimo cha bangi, watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola na kuchukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.Jabir Shekimweri
Aidha,Shekimweri amewataka wananchi wa Mpwapwa kuhakikisha wanafanya
kampeni kwa ustarabu na kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi
na kuwaonya watakaoleta vurugu kwamba watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
0 Comments