📌NA.FAUSTINE GIMU GALAFONI
MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mwalimu
Josephat Maganga ametoa rai kwa shirika
la elimu ya Amani Tanzania kuendelea kutoa elimu ya maadili na amani kwa watanzania ili
kuwajengea uwezo wa uzalendo na kulipenda taifa
lao.
Rai hiyo
ameitoa jijini Dodoma katika hafla fupi ya kongamano la shirika la Amani Tanzania hafla ambayo
imekutanisha viongozi mbalimbali wa shirika hilo linalojihusisha na kutoa elimu
ya amani hapa nchi tanzania ambapo mkuu
huyo wa wilaya amesema serikali
inatarajia mambo makubwa kutoka kwa shirika hilo .
Mmepewa jukumu kubwa katika zoezi la utoaji wa elimu ya mpiga kura pamoja na elimu ya amani kwa Taifa letu ,yapo mambo mengi ambayo tunatarajia kwenu hususan matarajio makubwa kutoka tume ya taifa ya uchaguzi hasa maadili yaliyosahihi kuelekea uchagui mkuu Oktoba 28,2020.
Mnapopeleka elimu ya maadili mpeleke kwa
uadilifu mkubwa ,sisi kama serikali tuna matarajio makubwa kutoka kwenu hivyo
muwafikishie walengwa elimu ya maadili kwani ninyi ni mabalozi wa tume ya taifa
ya uchaguzi”amesema.
Nao baadhi
ya viongozi wa shirika la elimu ya amani
Tanzania akiwemo rais wa shirika hilo,Wilson George ,naibu katibu mkuu
taifa Zailea Gogo,katibu mkuu elimu ya amani Zanzibar Ally Saleh Ally na mwenyekiti wa kongamano hilo Alex Kishimba
wameelezea miongoni mwa malengo ya shirika hilo kuwa ni pamoja na kutoa elimu ya
amani hapa nchini .
Rais wa shirika la Elimu ya Amani Tanzania,willson George Muunguza kulia akiwa na katibu mkuu Elimu Amani Zanzibar Ally Saleh Ally . |
Shirika la
elimu ya Amani Tanzania lilianzishwa rasmi mwaka 2017 kutoka kibali cha wizara ya mambo ya ndani na
mwaka 2019 lilipata usajili kutoka wizara ya afya maendeleo ya jamii,jinsia
,wazee na watoto na mwaka huu 2020 ni
asasi pekee ya kiraia iliyopewakibali na
serikali kupitia tume ya taifa ya uchaguzi kutoa elimu ya mpiga kura nchi nzima.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mwalimu Josephat Maganga akiwa upande wa kulia akifuatiwa na Naibu katibu Mkuu Taifa ,Shirika la Elimu ya Amani Bi.Zailea Gogo.
0 Comments