BAADA YA JPM: JUMUIYA YA MARIDHIANO WAUNGA MKONO UJENZI WA MSIKITI CHAMWINO




📌NA HAMIDA RAMADHANI

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge  kwa niaba ya   Rais  Dkt John Pombe Magufuli amemkabidhi  Meja Jenerali wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Charles Mbuge fedha za kitanzania Shilingi Milion 30 kutoka kwa wadau kwaajili ya ujenzi wa Msikiti Wilayani Chamwino.

Fedha hizo zilichangishwa siku ya jana katika Tamasha la Jumuiya ya maridhiano liliofanyika katika uwanja wa jamhuri Jijini hapa.


Akikabidhi fedha hizo kwa Meja Jenerali Mbuge katika ukumbi wa mikutano uliopo mkoani hapa,Dkt Mahenge amesema wadau mbalimbali wameendelea kujitokeza kutoa  michango yao na wengine kutoa ahadi za kuchangia ujenzi wa msikiti kuko Wilayani Chamwino.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum amesema Rais John Magufuli amefanya Jambo jema kwa wananchi wake wa dini ya Kislamu.

Kwa niaba ya Mufti mkuu wa Tanzania Shekhe Abubakari bin Zuberi nimeongea na amekiri  kwamba amefurahishwa na Rais Magufuli kuwatafutia wananchi wake nyumba ya Ibada na ameahidi kuja kutembelea 
Alhadi Salum.

Na kuongeza kusema " Tunamuombea Rais wetu awe na maisha marefu na wale wote wanaomuunga mkono na kumsaidia Rais wetu," Amesema.

Akiongea baada ya kukabidhiwa fedha hizo Meja Jenerali wa Jeshi la kujenga Taifa Charles Mbuge amewapongeza viongozi wa dini kuwa na upendo na mashikamano ya pamoja.

Amesema hiyo yote inatokana na Amani na utulivu tuliokuwa nao ndani ya Nchi yetu na ndio mana tunasali tunatembea tukiwa na Amani.

Naomba tu niseme tunaelekea kipindi Cha uchaguzi tudumishe Amani na mshikamano na tuwe pamoja na tumalize uchaguzi salama bila ya machafuko 
Meja Jenerali Mbuge.

Hata hivyo aliwataja wadau waliochangia Ujenzi huo wa Msikiti ni pamoja na Azim Dewji Mwenyekiti Kitosa Shia Ithna Shilingi Milion 10 keshi.

Abdul Zacharia,kutoka Abdul Zacharia Al Naeem Enterprise LTD ametoa Milion 20 taslimu.

Na Shekhe Arif Nahd Mwenyekiti Islamic Foundation ameahidi Shilingi Milion 10 na Jeshi la kujenga Taifa kuahidi shilingi milion 5


Post a Comment

0 Comments