📌NA.FAUSTINE GIMU
GALAFONI
Afisa nyuki Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania(TFS)Kanda
ya kati ,Bw.Karengi Slaa amebainisha
kuwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2002 ya ufugaji wa nyuki ni marufuku
kwa mtu yeyote kuuza asali kwenye vifungashio visivyo rasmi zikiwemo chupa za
konyagi ,chupa za bia na chupa zozote za Mafuta zilizokwisha tumika bila
kutoka moja kwa moja kiwandani.
Akizungumza na mtandao huu Agosti
26,2020 Bw.Karegi alibainisha kuwa kuuzia asali kwenye chupa ambazo
zilishatumika kuna weza sababisha madhara kwa mlaji hivyo ni vyema
wajasiriamali wa asali wakazingatia usafi kwa kuhifadhi asali katika ndoo na
chupa zilizotoka kiwandani moja kwa moja.
Katika suala la uuzaji wa asali katika chupa zilizotumika mfano katika chupa za konyagi,chupa za bia kwa kweli ni hatari kwa mlaji kwa hiyo nitoe rai tu kwa jamii kujitahidi sana kuwa na desturi ya kununua vifungajishio moja kwa moja kutoka kiwandani.Karengi Slaa
Afisa
huyo amesema kwamba unapochanganya asali
na chupa iliyokuwa na makaki ya bidhaa nyingine mfano,pombe na mafuta panaweza
kuleta madhara kwa mlaji.
Karengi
amesema kwa mujibu wa sheria ya mwaka
2002 ya ufugaji wa nyuki ni marufuku kwa mtu yeyote kuuza asali kwenye
vifungashio visivyo rasmi zikiwemo chupa za konyagi ,chupa za bia na chupa
zozote za Mafuta zilizokwisha tumika na na ikibainika fani yake ni Tsh.Milioni
1 au miezi sita jela au vyote kwa pamoja.
Pia,afisa nyuki mkuu huyo amesema kuwa huwa
wanafanya operesheni maalum kuhusu asali zinazochakachuliwa ikiwemo kuzidisha
kiwango cha maji.
Aidha,Slaa amebainisha kuwa TFS kanda ya
kati hadi sasa ina jumla ya Mashamaba ya asali 39 huku misimu ya urinaji wa zao
hilo muhimu hufanyika kwa misimu mikuu miwili ambayo ni Msimu mkuu
unaoanzia mwezi April hadi Julai na Msimu mdogo unaoanzia Mwezi Disemba hadi
Januari ya kila mwaka.
Katika kanda yetu ya kati ambayo inajumuisha mikoa ya Morogoro,Dodoma na Singida kufikia hadi sasa tuna jumla ya mashamba 39 ya asali ambayo yanasimamiwa na TFS mashamba yote hayo yametundikwa mizinga na mzinga mmoja una uwezo wa kutoa wastani wa kilo 7 hadi 9 za asali na ikumbukwe kuwa kuna aina mbili za asali ambazo ni asali ya nyuki wakubwa na asali ya nyuki wadogo na asali ya aina yote ni borakibiasharaKarengi Slaa.
Hata hivyo,amesema
kuhusu rangi ya asali huwa inategemea na aina ya mimea jinsi nyuki walivyokuwa
wanatafuta maua ili waweze kutengeneza asali ambapo pia alibainisha kuwa
asilimia 95% ya asali Tanzania inatokana na ufugaji asilia ambapo hutegemea
uoto wa asili ,ushauri wa wataalam na wafugaji wa jadi hutumia moshi
katika suala zima la urinaji wa asali.
Kuhusu suala la Elimu Bw.Slaa kati ya Wilaya
17 zilizopo kanda ya kati,Jumla ya wilaya 10 zilifikiwa kujengewa
uwezo juu ya namna bora ya ufugaji wa nyuki ambapo ni saw ana takriban
wajasiriamali 200 na asasi za kiraia zisizopungua 5 zikijengewa
uwezo huku mizinga 1000 ilisambazwa katika miaka mitatu iliyopita na mwitikio
ukiwa mkubwa.
Baraka Christopher ni Mkurugenzi wa kampuni ya
BEEKEEPING mkoani Dodoma inayojishughulisha na utoaji elimu ya nyuki
,akizungumza na mtandao huu katika semina iliyokutanisha Wajasiriamali
mbalimbali mkoani hapa mwanzoni mwa wiki katika ukumbi wa ofisi za
shirika la viwanda vidogovigogo (SIDO) amesema wao kwa kushirikiana na SIDO pamoja
na TFS wamefanikiwa kuwafikia wajasiriamali 40 mkoani hapa kutoa elimu ya
ufugaji bora wa nyuki huku akiwaasa watanzania kuchangamkia fursa ya ufugaji
huo kwani una tija kubwa.
Kwa kweli TFS,na SIDO wamekuwa mstari wa mbele kutupa support juu ya utoaji wa elimu ya ufugaji wa nyuki na tumefikia wajasiriamali 40 kutoa elimu na nyuki wanatengeneza asali ngundi Pamoja na sumu hivyo elimu ya ufugaji bora wa nyuki panakuwa na urafiki wa mazingira.Baraka Christopher
Nao baadhi ya wanufaika
wa mafunzo hayo na wajasiriamali wa nyuki mkoani Dodoma akiwemo
Sifa Lubasi,Damas Kambagu na Veronica Peter wamesema kuna umuhimu mkubwa kwa
wajasiriamali kupata mafunzo ya ufugaji bora wa nyuki na si kutegemea kuajiriwa
huku wakibainisha kuwa kuna baadhi ya vijana mkoani hapa huwa ni wavivu wa
kushiriki mafunzo lakini ni wepesi kuhudhuria masuala ya starehe hivyo ni
muhimu vijana kubadilika.
0 Comments