AAF YATOA MSAADA KWA FAMILIA YENYE WATOTO WATANO WENYE UALBINO



📌NA HAMIDA RAMADHANI

TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Albinism awereness Foundation (AAF)kwa kushirikiana na  Organisation For Social Support Initiatives and Enviroment (OSSIEC)
Wametoa msaada wa mahitaji kwa watoto watano wa familia moja wenye Ualbinism wenye thamani ya zaidi ya laki 9.

Akiongea kabla ya kukabidhi msaada huo Mkurugenzi wa AAF Suleiman Magoma amesema aliguswa  na kuona anahitajika kusaidia familia hiyo.
 Mara ya kwanza nilipokuja hapa nilikuja na rafiki angu  ambae ni Mkurugenzi wa Ossiec  Kennedy  Kassian nikaona mazingira wanayoishi nikaamua kuwashirikisha wafanyakazi wenzangu   maana niliona naguswa na nikiwatazama  naona wanafanana na mimi. 
Suleiman Magoma

Aidha msaada huo ni pamoja na kofia,miwani ya jua mafuta kwa ajili ya ngozi cherehani , telescopy kwa ajili ya kutumia kusoma wakiwa mbali na biashara ya genge kwa mama mwenye watoto kwaajili ya kujishughulisha ili aweze kujikwamua kiuchumi.

"Sisi kama Taasisi tutaendelea kuwafuatilia biashara namna inavyoenda tunakua kama walezi  na endapo itakwama tutaendelea kuwapa mawazo,"amesema Magoma

Naye Mkurugenzi wa Ossiec Kennedy Kassian amesema wao  waliona kumpa mtu chakula peke yake kwa mara moja haitoshi.
 Unapompa mtu chakula anakula kwa siku moja hujamsaidia bado kwasababu kitaisha  sisi tukaona ni bora tutoe kitu ambacho  ni tutaweka alama na msingi  wa maisha yao. 
Ossiec Kennedy Kassian

Kwa upande wake katibu wa Chama cha watu Wenye Ualbino Dodoma (TAS) Hudson Seme amesema kazi kubwa ya TAS  ni kufanya ushawishi na utetezi wenye haki kwa watu wote wenye Ualbinism ,kutoa elimu ya kiafya na elimu ya kidunia na kuwatambua na kuwaunganisha na fursa mbali mbali zinazojitokeza.
 Kikubwa ni upendo AAF imekua ikijitoa kwa kadri inavyoweza kwa kuhakikisha mtu yoyote mwenye ualibinism haachwi nyuma.
Hudson Seme

Hata hivyo Taasisi ya AAF ilianzishwa mwaka 2016 ikiwa na lengo la kuboresha hali za watu wenye ualibino Nchi.

Post a Comment

0 Comments