Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mahomanyika Enerst Kutona akiongea na Wakazi wa Mtaa huo waliofika eneo lenye mgogoro |
Wananchi wa Mtaa wa Mahomanyika kata ya Nzuguni jijini
Dodoma wameomba serikali kuingilia kati mgorogo unaendelea kati yao na kampuni
ya ujenzi ya China Henan International Cooperation Group (CHICO) juu ya eneo la mgodi wa madini ya ujenzi liliopo katika mtaa
huo.
Wananchi hao wanailalamikia kampuni hiyo kuvamia eneo katika
mtaa huo na kuanza kuchimba na kuchukua mchanga (kifusi) kwa ajili ya
ujenzi wa barabara katika mji mpya wa serikali (Mtumba).
Kwa mujibu wa Enerst Kutona ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali
ya mtaa huo uliopo nje kidogo ya mji wa Dodoma amesema hawana taarifa kuhusu
ujio wa kampuni hiyo na shughuli za uchimbaji wanzozifanya katika mtaa huo licha ya kupokea barua ya utambulisho.
Tulipokea barua kutoka TARURA ya kukutaka tuwape ushirikiano kampuni ya CHICO wakiwa wanatekeleza mradi wa barabara,lakini hatuna taarifa ya wao (CHICO) kufungua mgodi wa rasilimali za ujenziEnerst Kutona
Barua waliopokea Serikali ya Kijiji kutambulishwa kwa mkandarasi. |
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa wakazi wa mtaa huo
wanachohitaji ni kujua wanafaidika vipi na eneo hilo maana kampuni hiyo itaacha
mashimo katika eneo hilo baada ya ujenzi kumalizika.
Amesema licha ya kufanya jitihada mbali za wakuwasiliana na
malamla zinazohusika kujua uwepo wa mgodi huo wa mchanga na kokoti kwa ajili ya
ujenzi lakini hawajawahi kupata majibu.
Eneo ambalo kampuni ya CHICO inachimba mchanga katika mtaa huo |
Nae Nyemo Kiswagala ambaye ni moja wa wajumbe wa serikali ya mtaa huo amesema lengo
lao kubwa ni kutaka kufahamu wao wanafaidika vipi na uwepo wa kampuni ya CHICO
katika mtaa wao.
Lile eneo linachimbwa kifusi ni maeneo ya watu binafsi na ushahidi ni yale makaburi yaliyopo pale,kinachoniumiza CHICO hawajaja hata ofisini kujitambulisha na hata tulipowafuata wamesema hilo suala lipo chini ya TARURA ndio wanajua kila kitu na ukienda TARURA wanasema kazi wamempa CHICO yaani mwisho hatuelewi cha kufanyaNyemo Kiswagala
Mwandishi wetu alifika eneo hilo linalochimbwa mchanga huo
na kushuhudia baadhi ya wananchi wakiwa eneo hilo wakiomba ridhaa ya viongozi
wao kuyazuia magari hayo yasiendelee na kusomba mchanga huo hadi suluhu
itakapopatikana.
“Tunachotaka hapa wasitishe hii kazi kwa muda hadi
tutakapokubaliana.Tunataka kujua nani amekubaliana na huyo Mchina (CHICO) aje
kuvamia maeneo yetu na kuchimba kifusi wamefika kuanza kuchimba hadi makaburi
bila makubaliano na wanakijiji”-Amsema Felix Aidan mkazi wa Mahomanyika.
Malori ya kampuni ya CHICO yakisomba mchanga kutoka eneo hilo lenye mgogoro |
Kwa upande wake Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Ujenzi
ya CHICO Isaack Adrian amesema wao hawahusiki katika sakata hilo.
Meneja huyo amesema wao walipokabidhiwa kazi hiyo mteja wao
(TARURA) alienda kuwaonesha eneo hilo kwa ajili ya kupata mchanga (kifusi) kwa
ajili ya kujengea barabara za mji wa serikali ambazo zina urefu wa kilomita 40.
Mwandishi wetu pia alifika katika ofisi za TARURA
(Mtumba-Dodoma),akizzungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Taasisi hiyo (Alikuwa kwenye kikao cha bodi ya Manunuzi) Mhandisi Benjamini Magege amesema TARURA ina taarifa kuhusu mgogoro huo na wamejiandaa kukutana na pande zote akiwemo na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma
kuona namna bora ya kutatua mzozo huo.
0 Comments