📌NA DOTTO KWILASA
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma limepiga marufuku magari ambayo sio ya
viongozi na Ambulance kupiga ving’ora na kuahidi kuendelea kuwasaka madareva wote wanaokiuka agizo hilo.
Akizungumza na Waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa
Dodoma Gilles Muroto amesema Jeshi la Polisi limefanya msako na kufanikiwa kukamata magari 27
yaliyofungwa Ving’ora, vimulimuli,taa zenye mwanga mkali na zenye kubadilisha
rangi ikiwa ni kutekeleza agizo lilotolewa hivi karibuni na Mkuu wa Jeshi la
Polis nchini IGP Simoni Siro.
Muroto amesema kuwa IGP alishatangaza kupiga marufuku
gari yoyote ambayo siyo ya kiongozi wa Serikali, Ulinzi na Usalama, Zimamoto au
Ambulance kutumia alama hizo kwenye gari zao.
Aidha Muroto amesema gari
litakaloruhusiwa kutumia alama hizo ni ile ambayo imepata kibali maalumu kutoka Wizara ya Mambo
ya Ndani.
Magari hayo yaliyokamatwa yana kosa kisheria ya kwa kukiuka Kifungu 39(B) (1) (2) na kifungu cha 54(1)(2)(3)(4) na (5) cha Sheria ya Usalama Barabarani sura 168 ya mwaka 1973 na marejeo 2002Kamanda Muroto.
Katika hatua nyingine,Kamanda Muroto
amesema wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na gari aina ya Lori yenye namba za usajili T464
CGR ikiwa imepakia Drum 4 za nyaya za umeme aina ya ABC Conductor zenye ukubwa mita 3200 ambazo zinatumiwa na
Tanesco kusamabazia umeme.
Amesema wamefanikiwa kukamata gari hiyo
inayodhaniwa imebeba mali ya wizi Julai 15 saa 10 jioni katika Kijiji cha
Mbande Kata ya Sejeli Wilaya ya Kongwa katika barabara kuu ya Dodoma kuelekea Morogoro.
Baada ya kufanya uchunguzi wetu tulibaini watuhumiwa hao walikuwa wakisafirisha mzigo huo bila vibali wala risiti za manunuzi, na mbinu waliyotumia kuficha nyaya hizo chini ya mizigo ya bidhaa zingine za matumizi ya nyumbaniKamanda Muroto .
Muroto amewataja watuhumiwa hao kuwa ni
Ramadhani Mussa (25) mkazi wa Mkuyuni Mwanza, Athuman Abbas (22) mkazi wa
Bohari Mwanza na Shafii Mussa (23) Mkazi
wa Bohari Mwanza.
Kamanda Muroto amesisitiza watu kuacha
kuhujumu Uchumi kwani Serikali inajitahidi kuweka miundo mbinu kwa ajili ya kuwanufaisha Wananchi watu
wanahujumu.
0 Comments