📌NA DEVOTHA SONGORWA
Naibu Waziri huyo aliyasema hayo Jana
katika mkutano wa Baraza la Mawaziri wa nchi zinazozunguka Ziwa Victoria
uliofanyika kwa njia ya mtandao ikiwa ni njia ya kuendelea kupambana na virusi
vya Corona ukihusisha nchi za Kenya, Uganda, Burundi na Tanzania
ambapo alisema ajenda hiyo ni endelevu.
Amesema kwamba miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa
ni pamoja na kuiwezesha Taasisi ya Lake Victoria Fisheries Organization inatekeleza
majukumu yake katika hali ya ustawi kuendeleza sekta ya uvuvi katika nchi hizo ambayo imekuwa na mchango
mkubwa katika pato la taifa na kutoa huduma ya chakula kwa wananchi.
Sekta hii imekuwa na mchango mkubwa asilimia zaidi ya 60% ya mapato yanatoka katika Ziwa Victoria pia inawapatia watu ajira, chakula na hata biashara watanzania nao ni mashahidi nchi yetu inasafirisha minofu kutoka Mwanza kwenda nchi za Ulaya katika Ziwa Victoria hivyo hatuna budi kutumia raslimali hii vizuriUlega
Ameongeza kwamba Tanzania ni nchi ambayo ina eneo kubwa katika Ziwa hilo kuliko nchi
zingine hali ambayo inatoa chachu kwa watanzania kutumia fursa hiyo
kujiendeleza kiuchumi na kupambana na umaskini kundokana na maisha ya
utegemezi.
Akizungumzia mchango wa wananchi katika
sekta hiyo alieleza kwamba Tanzania ina wavuvi wasiopungua 200,000 ambayo wanajihusisha katika nyanja
mbalimbali huku wananufaika na mnyororo
wa thamani wakifikia zaidi ya milioni nne ikiwa ni azma ya serikali ya
awamu ya tano kutetea na kusimamia hali bora ya maisha kwa wananchi wake.
“Mchakato huu siyo kwamba utaishia kiazi
hiki tu tunafanya kwa ajili ya kizazi kijacho cha watoto wetu sasa serikali
haiwezi kufikia lengo hili peke yake bila kuunganisha nguvu na wananchi
kwasababu sisi ndiyo walinzi wa kwanza lazima tuwe na uchungu na vyetu kama
tunavyoona inatusaisia kuendesha maisha na kuinu auchumi wan chi yetu basi kila
mmoja aone ana cha kufanya kufikia matamanio yetu” Amesisitiza Naibu Waziri.
Ameleza kwamba baada ya mkutano huo yanatarajiwa
mabadiliko makubwa katika sekta ya Uvuvi kwa kila nchi kuona namna inavyoweza
kufanya kuendelea kutoa elimu kwa raia wake kuhusu manufaa ya Uvuvi akieleza
kwamba wanufaika wakubwa ni wananchi wenyewe
huku akiongeza kwmaba mkutano ujao unatarajiwa kufanyika nchini Kenya.
0 Comments