📌NA DEVOTHA SONGORWA
MKUU wa Tawi la
Utawala, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Kanali Julius Kadawi amewataka wahitimu
wa kidato cha sita kwa mwaka 2020
waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kuripoti katika makambi
walioyopangiwa kwa wakati ili kuanza mafunzo yanayotarajiwa kuanza nchini
August mosi mwaka huu.
Kanali Kadawi ameyasema
hayo jana jijini Dodoma wakati akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi
wa makao makuu ya jeshi hilo ambapo alisema kwamba vijana waliochaguliwa ni
kutoka shule zote za Tanzania Bara.
Jeshi limewapangia makambi watakayokwenda kupata mafunzo na wanatakiwa kuripoti kuanzaia tarehe 24 hadi 27 mwezi huu kwa sababu mafunzo hayo yatafunguliwa tarehe mosi 2020 hivyo ni vyema wakazingatia muda uliowekwaKanali Kadawi.
Ameongeza kuwa lengo
la mafunzo hayo ni kuwasaidia vijana kujifunza uzalendo,umoja wa kitaifa, stadi
za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa.
Akizungumzia wahitimu
wenye ulemavu wa kuonekan akwa macho aliwataka kuripoti katika kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi
mkoani Pwani ambayo imewekewa miundombinu ya kuhudumia watu wenye mahitaji
maalumu.
”Vijana waliochaguliwa
wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma mkoani Mara, JKT Msange mkoani Tabora,
JKT Ruvu mkoani Pwani, JKT Mpwapwa mkoani Dodoma, JKT Mafinga mkoani Iringa,
ikiwemo JKT Mlale iliyopo mkoani Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba iliyopo
mkoani Tanga.
Kambi zingine ni JKT
Makuyuni mkoani Arusha , JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila Imkoani
KIgoma , JKT Itanga mkoani Songwe, JKT
Luwa na JKT Milundikwa mkoani Rukwa sambamba na JKT Nachingwea iliyopo mkoani
Lindi, JKT Kibiti mkoani Pwani na Oljoro JKT iliyopo mkoani Arusha” Alizitaja
Kanali huyo.
Kufuatia uwepo wa
maambukizi ya virusi vya Corona nchini amesisitiz kwamba wamechukua tahadhali
za kujingika kupata maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu kama
zilizvyoelekezwa na serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kipindi chote vijana na watakapokuwa
katika mafunzo yao.
Katika hatua nyingine
Kanali Kadawi aliwataka waliochaguliwa kujiunga na mafunzo kutembelea tovuti ya
JKT ambayo ni www.jkt.go.tz ili kufahamu orodha kamili ya waliochaguliwa, vifaa
vinavyotakiwa na kambi walizopangiwa.
0 Comments