JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa
kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama limejipanga kudhibiti vitendo vya
utapeli kwa washiriki wa uchaguzi
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma , Gilles
Muroto amesema wamejipanga kudhibiti vitendo hivyo ili mkutano huo ufanyike kwa
usalama na amani
Jeshi limejipanga kuhakikisha yeyote atakayejaribu kufanya utapeli wa kujifanya yupo karibu na viongozi wakuu wa kitaifa hawataondoka Dodoma, wajipange kubakia ili kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria
RPC Muroto.
RPC Muroto amesisitiza kuwa hatotaka kuona vitendo vya utapeli katika mkutano
huo unaohudhuriwa na viongozi wakuu wa kitaifa, viongozi wa Serikali wastaafu,
viongozi wa vyama rafiki wa CCM kutoka mataifa mbalimbali duniani na kutoka
katika mikoa mbalimbali.
Muroto amesema mkutano huo unaotarajiwa
kuwa na wajumbe zaidi ya 3,000 hatopenda kuona watu wanatenda vitendo
vya kitapeli kwa kutumia ukaribu au majina ya viongozi.
Amesema uzoefu unaonesha katika mikutano
kama hiyo pia wamekuwa wakihudhuria watu
wenye nia ovu ambao wanatumia fursa hiyo kutekeleza azma yao ya kitapeli.
Muroto amesema jeshi hilo limejiandaa
kikamilifu kukabiliana na vitendo hivyo vya kitapeli kabla havijatokea .
0 Comments