📌NA BARNABAS KISENGI
Aliyekuwa diwani wa Kata ya Kizota jijini Dodoma kwa tiketi
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jamali Ngalya ameongoza katika kura za maoni
zilizofanyika katika Kata hiyo.
Ngalya ambaye ametia nia kutetea kiti chake katika kata hiyo
maarufu jijini hapa amepata kura 94 kati ya kura 112 kutoka kwa wajimbe wa
mkutano mkuu wa kata hiyo.
Mtia nia Bakari Juma ameshika nafasi ya pili baada ya kupata
kura 17 akifuatiwa na Peter Ngamangira aliyepata kura 1.
0 Comments