![]() |
Kaimu Mkurugezi wa
Sensa na Takwimu za jamii Ruth Minja
📌NA HAMIDA RAMADHANI
MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni,2020
umebaki kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Kaimu Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jimii
Ruth Minja amesema hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma kwa kwaka ulioishia mwezi
Juni 2020 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Mei
2020.
Amesema kuwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni
2020- kuwa sawa na mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020 umechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa bei
za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi
kilichoishia mwezi Juni 2020 zikilinganishwa na bei za mwezui Juni 2019.
Aidha ameongeza kusema kwamba ,Bidhaa za vyakula
zilizopungua bei kwa mwezi Juni 2020 zikilinganishwa na bei za mwezi Juni 2019
nipamoja na unga wa Maidi kwa asilimia 1.6 Matunda kwa asilimia 2.1,Viazi
mviringo kwa asilimia 5.0 ,mihogo kwa asilimia 13.3.
Kwa upande mwengine, amesema baadhi ya bidhaa zisizo za
vyakula ziliongezeka bei kwa mwezi Juni 2020 zikilinganishwa na bei za mwezi
Juni 2019 nipamoja na Mavazi kwa asilimia 2.7 ,Gesi ya kupikia kwa asilimia
7.8,Mkaa asilimia 11.2 ,Samani kwa asilimia 2.7 na Vitabu vyashule kwa asilimia
1.5.
Hata hivyo amesema Mfumuko wa bei wa bidhaa vya vyakula na
vinywaji barid kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umepungua hadi asilimia 3.8
kutoka asilimia 4.4 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020.
HALI YA MFUMUKO WA BEI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI.
Nchini Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni
2020 umepungua hadi kufikia asilimia 4.59 kutoka asilimia 5.33 kwamwaka
ulioishia mwezi Mei 2020,Kwaupande wa Nchi ya Uganda Mfumuko wa bei kwa mwaka
ulioishia mwezi Juni 2020 umeongezeka hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 2.8
kwamwaka ulioishia mwezi Mei 2020.
0 Comments