📌NA MUSSA ENOCK
Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma imeendelea na zoezi la uhamasishaji wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii ya CHF iliyoboreshwa lengo likiwa ni kutimiza adhma ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata matibabu kwa gharama nafuu.
Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma imeendelea na zoezi la uhamasishaji wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii ya CHF iliyoboreshwa lengo likiwa ni kutimiza adhma ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata matibabu kwa gharama nafuu.
Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo Dkt.Omary Nkulo amesema Halmashauri ya wilaya ya Kongwa ni moja ya Halmashauri ikifanya vizuri sana kwenye Bima ya CHF kutokana na mikakati ya
uhamasishaji waliojiwekea lakini pia ameahidi halmashauri hiyo kuendelea
kufanya uhamasishaji ili watu wengi zaidi wajiunge na Bima hiyo
Kongwa tumejiwekea utaratibu wa uhamasishaji,naipongeza sana timu yangu ya uhamasishaji chini ya Bwana Amos,inafanya kazi nzuri sana,sasa hivi tunakwenda kuhamasisha kwenye nyumba za ibada,na muitikio ni mkubwa sana.Dkt.Omary Nkulo
Akizungumza na wakina mama waliofika kwa ajili ya kupatiwa huduma ya
kliniki,mratibu
wa CHF Wilayani ya Kongwa Amos Ernest amewataka wananchi wa Kongwa kuchangamkia
fursa hiyo ya matibabu kwa gharama nafuu ya 30,000/= kwa kaya ya watu sita(6).
Amesema mpango huo wa CHF iliyobereshwa ni
juhudi za serikali ya awamu ya tano kuhakikisha Wananchi wanapata matibabu kwa gaharama hiyo nafuu, ili waweze kuepuka
usumbufu unaojitokeza wakati wa ugonjwa na kutafuta matibabu.
Mratibu huyo amesema kwamba kujiunga na Bima hiyo pia ni sehemu ya ushirikishwaji wa wananchi katika kuboresha huduma za afya katika wilaya hiyo.
Kwa mfano kituo chetu cha Afya Kibaigwa,mwezi Machi kimeweza kupata zaidi ya shilingi milioni mbili (2)hivyo pesa hiyo imewezesha hupatikanaji wa dawa wa uhakika katika kituoni.Amos Ernest
Kwa upande wake Neema Mazengo ambaye ni
miongoni mwa wananchi waliojiunga na Bima ya CHF aamesema kupitia Bima hiyo amekuwa akipata
huduma nzuri za afya bila usumbufu kila
anapofika kituo cha afya.
“Tangu nijiunge na Bima hii ya CHF mwezi Februari nimekuwa nikija hapa kituoni na kuhudumiwa vizuri,vipimo
na dawa vyote napata bure.Niwasihi tu wananchi wengine ambao bado hawajajiunga na CHF wajiunge, gharama ni nafuu sana.”Amesema.
0 Comments