![]() |
Wilfred Elisha Mgonera aliyeongoza kura za maoni Kata ya Pwaga,Mpwapwa |
📌NA BARNABAS
KISENGI
Diwani
aliyemaliza muda wake katika kata ya Pwaga jimbo la Kibakwe Wilayani Mpwapwa Vicent
Chawala ameshindwa kutetea kiti chake katika uchaguzi wa kura za maoni
zilizofanyika mwishoni mwa wiki wilayani humo.
Katika
Uchaguzi huo ambao Wilfred Elisha Mgonera aliibuka ‘kidedea’ kwa kuzoa kura 111,
Chawala ameshika nafasi ya nne (4) amepata kura 15 kutoka kwa wajumbe wa
mkutano huo.
Nafasi
ya pili imeshikwa na na Fadhili Mngoke aliyepata kura 22 na Harodi Mkombola
akishika nafasi ya tatu kwa ‘kuzoa’ kura 21.
Wagombea
wengine waliowania nafasi hiyo ni Fadhili amepata kura 15, Ashley Malolela (13),
Henry Kishimu (12), John Madee (6) na
Steven Mtuta (1) na Julius Lugodi (0).
👉👉👉SOMA HII:WAKAZI WA MAHOMANYIKA 'WAMJIA JUU' MKANDARASI BARABARA ZA MJI WA SERIKALI
0 Comments