330 WATIA NIA DODOMA, 57 WAJITOKEZA KUPAMBANA NA MAVUNDE



Ikiwa zoezi la uchukuaji na urejeshwaji wa fomu za kutia nia katika nafasi za Ubunge na Udiwani ndani ya Chama Cha Mapinduzi limefika tamati,mkoa wa Dodoma mambo yapo hadharani!

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbanga amesema  Wanachama 330 wamejitokeza kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya chama kuchaguliwa katika nafasi ya Ubunge katika majimbo 10 ya mkoa wa Dodoma.

Mbanga amesema hadi zoezi la kurejesha fomu hizo unafika tamati,waliojitokeza katika Majimbo 10 ni wanachama 324 ndio waliorejesha huku wanachama 6 wakishindwa kurejesha.

Katika jimbo la Dodoma mjini,wanachama 58 (Wanaume 52 na Wanawake 6).wamejitokeza kuchukua fomu za kuomba kupeperusha bendera ya CCM na wote wamerejesha fomu hizo.

Katika jimbo la Chemba waliojitokeza ni wanachama 33 (Wanaume 25 na Wanawke 8) na wote merudisha fomu zao.

Bahi waliojitokeza ni 36 (Wanaume 32 na Wanawake 4) na mmoja hajarudisha hivyo wanabaki 35 katika kuwania nafasi ya ubunge jimboni hapo.

Chamwino(Mtera) waliochukua fomu ni wanachama 18 (wote wanaume) na wote wamerejesha fomu zao.
Kondoa Mji,wanachama 47 wamejitokeza,na waliorejesha fomu ni 45 (Wanaume 42 na Wanawake 3) na wawili (2) hawajarudisha.

Amesema kwa upande wa UWT waliochukua fomu na kutia nia ni wanachama 97 na wote wamerejesha fomu zao.

  Kwa upande wa UVCCM wamejitokeza wanachama 28 na wote wamerejesha fomu na katika Jumuiya ya Wazazi  wanachama wawili (2) walichukua fomu na wote wamerejesha.

Post a Comment

0 Comments